UM waadhimisha Juni 12 ni siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto
Kila mwaka Juni 12 ni siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto na mwaka huu kauli mbiu ni "funga bao kutokomeza ajira ya watoto".
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika kuadhimisha siku hiyo imetoa wito wa hatua za haraka kuchukuliwa kote duniani ili kukata mirija ya ajira mbaya ya watoto.
UNICEF pia inasherehekea miaka kumi ya ushirikiano na shirika la IKEA katika kulinda haki za watoto na kupambana na ajira ya watoto. UNICEF inasema dola milioni 190 zilizotolewa kwa ushirikiano zimebadili maisha ya watoto wapatao milioni 100 katika nchi 30 na hivyo kuifanya UNICEF na IKEA kuwa wahisani wakubwa.