Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati kombe la dunia limeanza UM unasherekea uwezo wa michezo kuleta amani na maendeleo

Wakati kombe la dunia limeanza UM unasherekea uwezo wa michezo kuleta amani na maendeleo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amehudhuria sherehe za ufunguzi wa mashindano ya kombe la dunia nchini Afrika ya Kusini.

Hafla hiyo imehudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri, Rais wa FIFA Sep Blata, Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma na viongozi na wawakilishi kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo mamilioni ya washabiki wa kandandanda. Nderemo hizo na vifijo zimefanyika kwenye uwanja wa mpira wa Soweto mjini Johannesberg ambako mechi ya kwanza ya ufunguzi wa mashindano hayo baina ya wenyeji Afrika Kusini na Mexico imefanyika.

Mashindano haya yanafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika na yanajumuisha timu kutoka mataifa 32. Ban amehudhuria hafla hiyo baada ya kuhitimisha ziara yake nchini Cameroon ambako ameisifia nchi hiyo kama kiungo cha utulivu barani Afrika na kusisitiza kuwa malengo ya milenia yatafikiwa katika bara hilo hasa kwa kuongeza jitihada. Ameishukuru Cameroon kwa kuchangia vikosi vya polisi vya kulinda amani nchini Burundi, Kosovo, Haiti na Darfur.