Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ametoa wito wa kujerea utulivu Kyrgystan baada ya machafuko mapya

Ban ametoa wito wa kujerea utulivu Kyrgystan baada ya machafuko mapya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametoa wito wa kujerea kwa utulivu nchini Kyrigystan kufuatia taarifa za machafuko mapya yaliyosababisha vifo mjini Osh kusini mwa nchi hiyo.

Haya ni machafuko ya pili makubwa tangu kuondolewa madarakani Rais Kurmanbek Bakiyev mwezi aprili. Machafuko haya mapya yamekatili maisha ya watu 23 na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa na Rais wa muda ametangaza hali ya tahadhari.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake Bwana Ban amezitaka pande zote husika katika machafuko hayo kutulia na kuzuia kupotea zaidi kwa maisha ya watu.