WFP inaendelea kusaidia waathirika wa kimbunga Agatha Amerika ya Kati

WFP inaendelea kusaidia waathirika wa kimbunga Agatha Amerika ya Kati

Dhoruba kali imeathiri pakubwa mataifa ya Guatemala, Hondouras na El Salvador na kusababisha vifo vya watu 180, maelfu kuachwa bila makazi na uharibifu mkubwa.

Mkuu wa shirika la chakula duniani WFP Josset Sheeran amesema hali hii inakumbusha jinsi eneo hlo la Amerika ya kati lilivyo katika hatari hasa wakati huu wa kimbunga.

Ameongeza kuwa shirika hilo limetikitishwa na kupotea kwa maisha ya watu na adha wanazopata waathirika hususan wanawake na watoto. Ameongeza kuwa WFP inatoa msaada kwa maeneo yote yaliyoathirika ili kukabiliana na dhoruba hiyo.