Serikali zimetakiwa kusaidia kuwafikisha wahalifu mahakama ya kivita ICC:Ban

31 Mei 2010

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema, mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC) imefanikiwa kulazimisha serikali kubadili mwelekeo wao tangu iundwe miaka minane iliyopita.

Ban Ki-moon ameuambia mkutano unaofanyika Uganda unaojadili kuhusu mahakama hiyo iliyopo Hague kwamba imepunguza uwezekano wa watu kuepuka adhabu na kuweka misingi mipya juu ya haki za waathiriwa. Lakini ametoa wito wa nchi wanachama kushirikiana.

ICC ina kesi tano zinazoendelea, zote zikiwa kutoka barani Afrika. Mpaka sasa hakuna aliyepatikana na hatia ya madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita. Bw Ban aliwaambia viongozi, " Kwa wakati ule wachache wangeamini kwamba mahakama hii ingekuwa hapa ilipo, inafanya kazi vizuri, inafanya utafiti na kuendesha mashtaka ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

"Katika karne hii mpya ya uwajibikaji, wale wanaofanya uhalifu mkubwa zaidi dhidi ya binadamu watashughulikiwa ipasavyo." Bw Ban amesema wakati sasa umepita wa dunia kuchagua baina ya amani na haki- sasa mataifa yanatakiwa kukabiliana nayo bega kwa bega.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter