Ban akubali mwaliko wa kwenda kwenye ufunguzi wa kombe la dunia

Ban akubali mwaliko wa kwenda kwenye ufunguzi wa kombe la dunia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ameridhishwa na mwaliko binafsi aliopewa kwenda kuhuduria sherehe za ufunguzi wa kombe la dunia nchini Afrika ya Kusini 11 juni mwaka huu.

Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa, Martin Nersiky Katibu Mkuu amepokea mwaliko huo kutoka kwa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma na Rais wa FIFA, Sepp Blatter.

Katibu Mkuu amesema kufanyika kwa kombe hilo nchini Afrika ya Kusini ni uthibitisho tosha wa uwezo wa nchi hiyo na bara zima la Afrika kwa ujumla. Amesema ni fursa kubwa kwenye mashindano hayo kutafakari malengo ya milenia.