Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa kuwaenbzi walinda amani kote duniani katika siku maalumu

Umoja wa Mataifa kuwaenbzi walinda amani kote duniani katika siku maalumu

Tarehe 29 Mai ni siku maalumu ya kimataifa na Umoja wa Maita ya walinda amani. Siku hii uadhimishwa kila mwaka ili kuwaenzi watu mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia wanaoshiriki shughuli za kulinda amani katika mataifa mbalimbali.

Pia siku hii ni kuwakumbuka waliopoteza maisha yao katika vikosi hivyo vya kulinda amani.

Kuthamini mchango wao na juhudi zao za kuhakikisha dunia inakuwa mahali bora pa kuishi.

Tukikaribia siku hiyo tunakuletea taarifa mbalimbali kutoka kwa watu wanaoshughulika na mpango huo.

Na leo tunaye Emmanuel Mollel mkuu wa maji na ulinzi wa mazingira Darfur kwenye kikosi cha UNAMID anasema umuhimu wa siku hii.