Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa tathimi ya mahakama ya uhalifu wa kivita ICC kufanyika Uganda

Mkutano wa tathimi ya mahakama ya uhalifu wa kivita ICC kufanyika Uganda

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon katika mkutano waliouiita wakati wa Uwajibikaji, amesisitiza umuhimu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC na mkutano wa kutathimini mahakama hiyo utakaofanyika mwishoni mwa wiki nchini Uganda.

Ban amesema ni fursa nzuri sio tuu kutathimini hatua zilizopigwa bali pia kwa ujuenzi wa siku zijazo. Ameongeza kuwa pia ni wakati wa kuimarisha juhudi za pamoja za kuhakikisha kwamba makosa dhidi ya ubinadamu hayaachwi bila kuchukuliwa hatua.

Amesema wakati wa kufumbia macho uhalifu umepita na taratibu wakati wa uwajibikaji unazaliwa. Amesema walianza na mahakama ya mauaji ya kimbari ya Rwanda, kisha ya Yugoslavia ya zamani na sasa ni ICC. Hata hivyo balozi wa Uganda kwenye Umoja wa Mataifa Ruhakana Rugunda amesema kuna baadhi ya mambo ya ICC yanatia shaka hususani Afrika.