Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban yuko Brazili kuhudhuria mkutano wa muungano wa ustaarabu

Ban yuko Brazili kuhudhuria mkutano wa muungano wa ustaarabu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amewasili Rio de Janeiro leo kabla ya mkutano wa muungano ustaarabu ambao utafunguliwa hapo kesho.

Shughuli hizi zitampa nafasi ya kujionea kwa ukaribu maendeleo yaliyopigwa na nchi ya Brazil katika kuangamiza umaskini pamoja na kufikia malengo ya milenia.  Baadae Ban atatembelea mitaa ya mabanda Rio de Janeiro ambapo atakutana na vijana na watu wengine wanaoishi katika mitaa ya mabanda karibu na mji wa Rio de Janeiro ili kusikia moja kwa moja kutoka kwao ukweli wa hali halisi kuhusiana na huduma na nafasi katika muktada wa malengo ya milenia.

Mkutano huu utafuatiliwa na mkutano mwingine na familia za wanajeshi wa kulinda amani ya Umoja wa Mataifa ambao waliuwawa wakati wa tetemeko la ardhi pamoja na kuzindua alama ya makumbusho ya wanajeshi hao.