Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjadala wafanyika canada juu ya ulinzi wa kimataifa wa wakimbizi

Mjadala wafanyika canada juu ya ulinzi wa kimataifa wa wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeanzisha mjadala mkubwa kuhusu mkazo wa kiwango cha kimataifa cha ulinzi.

Mkurugenzi wa UHNCR Volcker Turk akizungumza kwenye mkutano mjini Toronto Canada amesema njia muhimu ya utekelezaji wa kiwango cha kimataifa cha ulinzi kwa wakimbizi utategemea na jinsi UNHCR itakavyokuwa na viwango vya juu vya uchunguzi na usimamizi wa ulinzi wa kimataifa.

Amesema mkutano huo ni mfursa nzuri kujadili mada hiyo, na amewajulisha wanazuoni na wanasheria wanaohudhuria kuwa juhudi za UNHCR za kusimamia kiwango cha kimataifa cha ulinzi wa wakimbizi ni moja ya hatua muhimu kuwalinda wakimbizi duniani.