Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUC inawasaidia waathirika wa maporomoko ya ardhi DRC

MONUC inawasaidia waathirika wa maporomoko ya ardhi DRC

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUC wamekuwa wakitoa msaada kwa raia wa nchi hiyo walioatghirika na maporomoko ya ardhi.

Kwa kutumia magari yanayohilimi hali mbaya wanajeshi wa MONUC wamekuwa wakipeleka misaada na kuwahamisha watu baada ya mvua kubwa kusababisha mto kufurika na kuleta maporomoko ya ardhi kusini mwa nchi hiyo.Hadi sasa watu 46 wameuawa kutokana na maporomoko hayo, nyumba zaidi ya 200 kuharibiwa na maelfu ya watu kuachwa bila makazi.

Msemaji wa MONUC Madnoje Mounoubai ameliambia shirika la habari la Umoja wa Mataifa kwamba leongo lao ni kuwalinda raia hadi mashirika ya misaada yatakapowasili. Hadi sasa MONUC imefanikiwa kuopoa maiti 16 zilokuwa zimefukiwa na tope karibu na mlima Nyiragongo mjini Goma kwenye mkoa wa Kivu ya Kaskazini.