Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfuko wa kimataifa umezindua kampeni ya watoto kuzaliwa bila HIV

Mfuko wa kimataifa umezindua kampeni ya watoto kuzaliwa bila HIV

Mfuko wa kimataifa (Global Fund) leo umezindua kampeni iitwaayo ‘kuzaliwa bila HIV\' kampeni inayoungwa mkono na mke wa Rais wa Ufransa Carla bruni Sarkozy.

Kampeni hiyo ni ya kuchagiza umma kuunga mkono juhudi zake na za dunia za kuhakikisha watoto wanazaliwa bila kuwa na virusi vya HIv ifikapo mwaka 2015. Kampeni hiyo ambayo imeanzishwa na kuungwa mkono na Carla Bruni sarkozy ambaye ni balozi mwema wa Global fund itahusiha vitu mbalimbali ikiwemo filamu fupi yenye lengo la kuwashawishi watu kuunga mkono mpango wa mfuko huo kupitia mtandao.

Kampeni hiyo pia itatumia miundo mbalimbali kufikisha ujumbe na kuyaleta pamoja makampuni makubwa ambayo yamesaini rasmi kuwa wshirika na kuunga mkono mfuko wa kimataifa yakiwemo Google, JC Decaaux, Jean Paul Gaultier, MSN, Orange, Tiffany &Co na You Tube ambayo itakuwa uwanja muhimu wa kampeni hiyo.