Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikao cha 63 cha kimataifa cha afya kimeanza leo mjini Geneva

Kikao cha 63 cha kimataifa cha afya kimeanza leo mjini Geneva

Mkutano wa 63 wa kimataifa wa afya umeanza leo mjini Geneva. Mkutano huo unaanza wakati shirika la afya duniani WHO likiadhimisha mwaka wa 30 tangu kufanikiwa kutokomeza ugonjwa wan dui.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo mkurugenzi mkuu wa WHO Dr Margaret Chan amesisitiza kwamba afya ya jamii daiama inatakuiwa kupiga hatua kutokana na mafanikio na kasoro zilizopo.

Amesema mafanikio kama ya kutokomeza ndui ni ishara tosha kwamba dunia ikiungana pamoja hakuna lisilowezekana. Lakini amesisitiza juu ya malengo ya milenia kwamba juhudi zinahitajika kwani muda uliosalia ni mdogo