Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhusiano wa simu za mkononi na saratani wahitaji utafiti zaidi:WHO

Uhusiano wa simu za mkononi na saratani wahitaji utafiti zaidi:WHO

Utafiti mkubwa uliofanywa na shirika la afya duniani kuhusu uwezekano wa uhusiano baina ya matumizi ya simu za mkononi na aina Fulani za saratani ya ubongo haujapata jibu lililowazi.

Watafiri wanasema matokeo yanaonyesha kuwa kuna uwezekano wa athari za kiafya kutokana na matumizi makubwa ya simu za mkononi, lakini wanasema utafiti zaidi unahitajika ili kupata matokeo yaliyo dhahiri.

Utafiti huo uliochukua miaka kumi na kuwalenga watu 13,000 umekosolewa kwa sababu makampuni ya simu ndiyo yaliyofadhili asilimia 25 ya utafiti huo.