Skip to main content

UNDP na serikali ya Norway wabainisha vifo vitokanavyo na vita vya silaha

UNDP na serikali ya Norway wabainisha vifo vitokanavyo na vita vya silaha

Zaidi ya watu 74,000 wanafariki dunia kila mwaka kwa ajili ya mapigano ya kutumia silaha, huku wengine 2,000 wakipoteza maisha kila siku.

Takwimu hizi ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP na wizara ya mambo ya nje ya Norway, katika juhudi zao za kutoa kipaumbele katika upunguzaji wa mapigano ya kutumia silaha katika Nyanja ya maendeleo ya kimataifa.

Wajumbe kutoka nchi 60, mashirika ya kimataifa na makundi yasiyo ya kiserikali wanatarajiwa kutia saini azimio la juhudi zinazochangia kupunguza vita vya silaha ambavyo ni kikwazo kikubwa cha kufikia malengo ya milenia. Paul Eavis ni mshauri wa kitengo cha kuzuia vita vya kutumia silaha wa UNDP (CLIP Eavis).