Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa CSD wiki ijayo kuchagiza juhudi za kupatikana maendeleo endelevu

Mkutano wa CSD wiki ijayo kuchagiza juhudi za kupatikana maendeleo endelevu

Washiriki wa mkutano wa ngazi ya juu wa kamati ya rasilimali utakaofanyika wiki ijayo watajenga utashi ili kuharakisha juhudi za kupatikana kwa maendeleo endelevu.

Lengo hilo limetolewa na mwenyekiti wa tume ya maendeleo endelevu ya Umoja wa mataifa (CSD) ambaye pia ni waziri wa mazingira na rasilimali wa Guatemala Luis Alberto Ferrate.

Mkutano wa CSD unaoendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York unaangazia masuala matano likiwemo la usafiri, usimamizi wa taka na madini.

Akizungumza na waandishi wa habari bwana Ferrate amesema wateja wanazingatia masuala ya mazingira na jamii.