Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umezitaka nchi za Ulaya kuwa wabunifu kutokomeza umasikini

UM umezitaka nchi za Ulaya kuwa wabunifu kutokomeza umasikini

Umoja wa Mataifa unatumai kutumia ubunifu wa Ulaya kuchagiza ujumbe wake kwa nchi za eneo hilo kuhusu malengo ya milenia (MDG\'S) hususani lengo la nane ambalo ni kutokomeza umasikini ifikapo mwaka 2015.

Umoja wa Mataifa umeanza kampeni ya matangazo ikiwakaribisha raia wote wan chi 48 za Ulaya na hata wataalamu wa matangazo kuwasilisha ukurasa mmoja ambao unaweza kuwa ni michoro, picha, vikaragosi au ujumbe.

Mkurugenzi wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa mjini Brussels (UNRIC) ambaye alizindua kampeni ya shindano kwenye wavuti amesema moja ya malengo ya shindano hilo ni kuwa na ushirikino na magazeti ya Ulaya.

Mshinindi atapata zawadi ya Euro 5000 kutoka kwa serikali ya Hispania kwenye hafla itakayofanyika mjini Madrid, kabla ya mkutano wa MDG'S utakaoanza mjini New york mwezi Septemba.