Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafiri imara ni muhimu katika kuchangia maendeleo ya nchi yoyote

Usafiri imara ni muhimu katika kuchangia maendeleo ya nchi yoyote

Kikao cha tume ya maendeleo endelevu kinachofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York kimejadili suala la usafiri na mazingira.

Kikao hicho kimesema japo uepesi wa usafiri na kuvuka mipaka ni muhimu katika ukuaji wa uchumi maendeleo ya jamii na biashara ya dunia, mara nyingi inachangia katika uharibifu wa mazingira. Amesema afisa wa ngazi ya juu wa kitengo cha uchimi na masuala ya jamii wa Umoja wa Mataifa .

Kathleen Abdala katika ripoti yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema baadhi ya changamoto mpya ambazo zimezuka mwaka 200 ni pamoja na soko la dunia la nishati kubadilika kila wakati, kupungua kwa mahitaji ya binadamu na huduma kufuatia kuporomoka kwa soko la fedha duniani, na haja ya kupunguza gesi inayoharibu mazingira.