Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za Asia na Pacifiki zatakiwa kuongeza matumizi ya kijamii kuchepusha uchumi

Nchi za Asia na Pacifiki zatakiwa kuongeza matumizi ya kijamii kuchepusha uchumi

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa siku ya Alhamisi imezihimiza serikali za Asia na Pacific ziongeze matumizi ya kijamii ili kukabiliana na matatizo ya kiuchumi ambayo hayakutarajiwa.

Riporti ya Kamishana wa Umoja wa mtaifa ya Asia na Pacific (ESCAP) inasema kuongezwa kwa fedha katika sekta ya kijamii kutasaidia katika ukuaji wa uchumi.

Katika hafla ya kuzinduliwa kwa riporti hiyo nchini Thailand, mkuu wa ESCAP, Noeleen Heyzar ameonya kuwa kando na kwamba maeneo ya Asia na Pacif yamekuwa kiuchumi kuna masuala mengine ambayo yanafanya mwaka wa 2010 kuwa ngumu kwa watunga sera.