Skip to main content

UNHCR sasa imeweza kuwafikia wakimbizi 35,000 wa walioko Congo Brazaville

UNHCR sasa imeweza kuwafikia wakimbizi 35,000 wa walioko Congo Brazaville

Wafanyakazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wamepata fursa ya kuwafikia wakimbizi 35,000 wa Jamhuri ya Congo walioko kando mwa mto Oubangui.

Wakimbizi hao ni sehemu ya wakimbizi 114,000 waliokimbia mapigano yaliyochagizwa na masuala ya uvuvi na kilimo kwenye jimbo la Equateir kaskazini magharibi mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo oktoba mwaka jana.

operesheni za jeshi la Jamuhurui ya Kidemokrasia ya Congo za kuwasaka waasi kwenye jimbo la Equateur zilizuia wafanyakazi wa misaada kuwafikia wakimbizi hao kwa wiki tano zilizopita, lakini kuondolewa kwa vikwazo vya usalama sasa wafanyakazi wa UNHCR wameweza kuwafikiwa wakimbizi hao.