Skip to main content

Matatizo yanayoendelea Somalia yanawapa adha kubwa jirani zake

Matatizo yanayoendelea Somalia yanawapa adha kubwa jirani zake

Ujumbe wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR uliozuru makambi ya wakimbizi wa ndani wa Somalia umeshuhudia adha inayowakabili watu hao.

Ujumbe huo ulioongozwa na naibu kamisha wa UNHCR umetathimini ongezeko la msongamano wa wakimbizi na upungufu wa huduma muhimu katika makambi ya Ethiopia, Djibouti, Kenya na ndani ya Somalia kwenyewe.

Miongo miwili ya vita Somalia imewalazimisha Wasomali milioni mbili kuzikimbia nyumba zao wengine kwenda nchi jirani za Kenya, Ethiopia, Djibouti na yemen na walioshindwa kusalia katika maeneo yenye usalama nchi Somalia na kuwa wakimbizi wa ndani.