Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa walaani shambulio la bomu Moghadishu mwishoni mwa wiki

Umoja wa Mataifa walaani shambulio la bomu Moghadishu mwishoni mwa wiki

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia , Ahmedou Ould-Abdallah amelaani vikali mashambulio ya bomu mjini Mogadishu yaliyotokea mwishoni mwa wiki na kuua Wasomali na raia wa kigeni.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo takribani watu 30 wameuawa na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa kwenye mripuko uliotokea msikitini.

Bwana Ould-Abdallah amesema hili lilikuwa ni shambulio la kikatili dhidi ya watu waliokwenda msikitini kuswali. Amewataka Wasomali kuacha mashambulio hayo na kutafuta amani kwa maslahi ya yao, watoto wao na taifa lao.