Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa haki za binadamu anasema kuna haja ya ushirikiano kutekeleza haki

Mkuu wa haki za binadamu anasema kuna haja ya ushirikiano kutekeleza haki

Kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay amesema kuna haja ya kuwepo na ushirikiano zaidi kukabiliana na changamoto za haki za binadamu kote duniani.

Pillay ametyasema hayo wakati wa ufunguzi wa warsha ya kimataifa ya kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika kuchagiza na kulinda haki za binadamu iliyoanza leo.

Bi Pillay ameainisha kuwa ofisi yake imechukua hatua kadhaa zenye lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya mfumo wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa mipango ya kikanda.