Skip to main content

Ban ameyataka mataifa yote kutimiza malengo ya kuachana na nyuklia

Ban ameyataka mataifa yote kutimiza malengo ya kuachana na nyuklia

Mataifa zaidi ya 100 yanakutana kwenye makao makuu ya Umoja wa mataifa kwa ajili ya mkutano wa kupinga uzalishaji wa silaha za nyuklia.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amefungua mkutano huo na tangu aliposhika wadhifa wa Katibu Mkuu  wa Umoja wa Mataifa mwaka 2007 upokonyaji wa silaha za maangamizi imekuwa moja ya malengo yake makubwa. Ban amesema kuwa na dunia huru bila silaha za nyuklia ni jambo linalopewa kipaumbele na Umoja wa Mataifa na ni muhimu kwa maisha ya binadamu.

Wengine watakaozungumza katika mkutano huo wa mkataba wa kupinga uzalishaji wa nyuklia NTP ni mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA Yukiya Amano na Rais wa Jamhuri ya watu wa Iran Mahmoud Ahmadinejad.