Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari

Leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari

Leo dunia nzima inaadhimisha siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari. Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni "uhuru wa kupata taarifa" kauli ambayo inatukumbusha umuhimu wa haki ya kujua kinachoendelea.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema waandishi wengi wa habari wanapoteza maisha, wengine kugungwa, kupata vitisho kwasababu tuu wanatimiza haki yao ya kutafuta, kupokea na kupasha habari, amezitaka nchi zote kuzingatia haki ya uhuru wa vyombo vya habari.

Naye mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la sayansi, elimu na utamaduni UNESCO Irina Bokova katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku hii amesema uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu na ni haki ya watu kupata taarifa.