Waathirika wa vita katika bonde la Swat Pakistan bado wana dhiki

30 Aprili 2010

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema mwaka mmoja baada ya machafuko ya bonde la Swat Pakistan maelfu ya waathirika bado wanahangaika kujenga upya maisha yao.

UNHCR imeonya kwamba wkimbizi wa ndani bado ni tatizo kubwa katika bonde la Swat na wilaya zingine ambako watu zaidi ya milioni mbili walilazimika kuzikimbia nyumba zao.

Kwa mujibu wa serikali ya Pakistan asilimia 80 au 90 ya watu waliokimbia wamerejea kwenye maeneo yao, lakini shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA limesema Pakistan inakabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha, jambo linaloweka katika hatihati shughuli za misaada kwenye jimbo la mpakani la Kaskazini Magharibi na la FATA, MAHECIC ni afisa wa OCHA.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter