UNHCR yataka muungano wa Ulaya kuwa mfano wa kuwalinda wakimbizi

UNHCR yataka muungano wa Ulaya kuwa mfano wa kuwalinda wakimbizi

Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Antonio Guterres amezitaka nchi 72 za muungano wa Ulaya kuwa mfano mzuri wa kuwalinda wakimbizi.

Katika mjadala uliofanyika jana na wajumbe wa bunge la Ulaya Bwana Guterres amesema kwamba muungano wa Ulaya ambao mipaka yake ya ndani imetoweka watu wanaoomba hifadhi waweze kupata hifadhi hiyo kila wanapoomba.

Ameongeza kuwa Muungano wa Ulaya unahitajika kujitahidi kuangalia upya mfumo wake wa kuomba hifadhi ili iweze kuwasaidia wakimbizi hao.