IAEA na Roche kusaidia vita dhidi ya saratani kusini mwa jangwa la Sahara

IAEA na Roche kusaidia vita dhidi ya saratani kusini mwa jangwa la Sahara

Shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA linashirikiana na Roche shirika linaloongoza katika matibabu ya saratani, kukabiliana na ongezeko la matatizo ya saratani katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara.

Wakati mzigo wa magonjwa ya saratani unaongezeka katika nchi zinazoendelea kuna haja kubwa ya wataalamu wa afya, hosipitali na huduma za matibabu.

Katika kukabiliana na hali hiyo IAEA na Roche wanafanya kazi pamoja ili kusaidia hasa katika kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya barani Afrika.