Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upimaji wa saratani kwa kutumia mionzi unawaweka watoto katika hatari

Upimaji wa saratani kwa kutumia mionzi unawaweka watoto katika hatari

Wakati huohuo utafiti wa kimataifa uliofanywa na shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA unaonyesha kuwa katika baadhi ya nchi watoto wanawekwa katika hatari kubwa ya mionzi wanapofanyiwa vipimo kama CT scans.

Utafiti huo unasema watoto wanapata mionzi kwa kiwango cha watu wazima, licha ya wataalamu kuonya juu ya vipimo hivyo kwa muda mrefu.

Utafiti huo uliofanyika katika vituo vya afya 128 kwenye nchi 28 barani Afrika, Asia na Ulaya Mashariki pia umeonyesha kuwa kuna tofauti kubwa ya viwango vya mionzi na idadi ya vipimo vya CT sacan vinavyofanywa kwa watoto wa chini ya umri wa miaka 15.