Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kimataifa ya afya na usalama katika maeneo ya kazi

Leo ni siku ya kimataifa ya afya na usalama katika maeneo ya kazi

Leo ni siku ya kimataifa ya masuala ya afya na usalama kazini. Katika kuadhimisha siku hii mkuu wa shirika la kazi duniani ILO ametoa wito wa kuzuia hatari zozote zinazojitokeza katika sehemu za kazi.

Juan Somavia amesema siku za kuafanya kazi zinapotea, matibabu yahahitajika na fedha nyingi zinapotea kutokana na ajali zinazotokea kazini au majeraha, ambazo ni sawa na asilimia 4 ya mapato. Ameongeza kuwa tuanakabiliwa na athari za ajali zilizotokea kazini siku za nyuma.

Watu milioni 2.3 wanakufa kutoka na majeraha au magonjwa yanayoambatana na ajali hizo kila mwaka. Na wakati huohuo tunakabiliwa na changamoto afya na usalama kazini katika dunia hii inayokabiliana na mabadiliko ya haraka.