Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asisitiza kufufua maeneo yaliyoathirika na zahma ya Chernobly

Ban asisitiza kufufua maeneo yaliyoathirika na zahma ya Chernobly

Leo ni miaka 24 tangu kutokea zahma ya nyuklia ya Chernobly ambayo mionzi yake imewaathiri watu zaidi ya milioni nane Belarus, Ukraine na Urusi.

Katika kumbukumbu hiyo leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amerejea wito wake na kusistiza kuwa ni muhimu kuyafufua maeneo ya nchi hizo tatu ambayo hadi leo mbado yanahangaika kukabiliana na athari za zahma ya Chernobyl.

Katika taarifa yake Ban amesema tunawakumbuka mamia ya wahudumu wa dharura waliofika kusaidia katika ajali hiyio, zaidi ya watu 330,000 waliofariki dunia na maelfu ya watoto ambao badaye walijikuta wakipata saratani.

Ameitolea wito jamii ya kimataifa kufanya kila iwezalo kufufua maeneo yaliyoathirika miaka 24 iliyopita na kuwasaidia watu ambao bado wako katika athari za nyuklia hiyo.