UNAIDS imeitaka serikali ya Ukraine kuhakikisha huduma kwa waathirika wa HIV

UNAIDS imeitaka serikali ya Ukraine kuhakikisha huduma kwa waathirika wa HIV

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya HIV na Ukimwi UNAIDS limesema linahofia taarifa ya uchuguzi wa serikali ya Ukraine dhidi ya mtandao unaowasaidia watu wanaoishi na virusi vya HIV uitwao All-Ukrainian Network na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali yanayoshughulika na ukiwmi nchini humo.

UNAIDS imeitaka serikali ya Ukraine kuhakikisha kwamba uchunguzi huo hautasababisha kuingiliwa kwa huduma za HIV zinazotolewa na mashirika hayo kwa maelfu ya watu. George Njogopa anaripoti.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)