Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa Kimataifa wa Uhalifu umemalizika nchini Brazil

Mkutano wa Kimataifa wa Uhalifu umemalizika nchini Brazil

Mkutano wa kimataifa uliokuwa ukijadili uhalifu na masuala ya sheria umemalizika leo Bahia nchini Brazili. Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa ofisi inayohusika na dawa za kulevya na uhalifu amesema uhalifu uliopagwa na kuhusisha watu wengi ndio tishio kubwa katika usalama na maendeleo.

Katika hitimisho la mkutano huo ambao ni kongamano la 12 la Umoja wa Mataifa la kuzuia uhalifu na makosa ya jinai Salvador Bahia Brazili Antonio Maria Costa amewaambia washiriki wa kongamano hilo kwamba uhalifu uliopangwa na magenge ni mkubwa na ni tishio linalohitaji suluhu ya haraka..