Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu ni ufunguo katika mapambano dhidi ya Ukimwi yasema UNICEF

Elimu ni ufunguo katika mapambano dhidi ya Ukimwi yasema UNICEF

Mkurugenzi anayeondoka wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF amesema elimu ni muhimu sana katika vita dhidi ya Ukimwi.

Ann M Veneman ameyasema hayo wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Lesotho, nchi ambayo ni ya tatu duniani kuwa na idadi kuwa ya maambukizi ya HIV. Bi Veneman ambaye alizuru miradi mbalimbali ya afya na kujionea hali halisi na athari za Ukimwi nchini Lesotho ambako umri wa kuishi umepungua hadi miaka 40, amesisitiza kuwa elimu iwe kitovu katika vita dhindi ya kuenea kwa ukimwi.

Amesema nchi hiyo ina idadi kubwa ya watoto yatima na walio katika hatari wengi wao wamepoteza mzazi mmoja au wote kutokana na Ukimwi. Ameongeza kuwa UNICEF inashirikana kwa karibi na washirika wake na serikali ya Lesotho kuhakikisha kwamba watoto wa nchi hiyo wanapata huduma ya afya inayotakiwa na elimu.