Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya afya duniani, WHO inasema afya mijini ni muhimu sana

Leo ni siku ya afya duniani, WHO inasema afya mijini ni muhimu sana

Leo ni siku ya afya duniani na kauli mbiu ya mwaka huu inasema "afya mijini ni muhimu sana".

Katika kuazimisha siku hii shirika la afya duniani WHO limezindua kampeni ya kuifanya miji kuwa na afya bora. Katika kampeni hiyo WHO inatoa wito kwa viongozi wa miji kuwajali wakazi wake kwa kuwaelimisha juu ya maisha bora yanayozingatia misingi ya afya na pia kuangalia mapungufu yaliyopo mijini katika mfumo wa afya na kuyafanyia kazi.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Dr Margaret Chan amesema ingawa bado kuna mapungufu lakini kwa ujumla watu wa mijini wana afueni kiafya kuliko wa vijijini, kwani wengi wanaweza kupata huduma za afya kwa uraisi, wamesoma na umri wao wa kuishi ni mrefu zaidi kuliko vijijini.

Lakini amesema kuboresha afya mijini ni muhimu sana kwani kila siku maelfu ya watu wanahamia mijini.