Umoja wa Mataifa umeomba fedha zaidi kusaidia waliokumbwa na njaa Niger

5 Aprili 2010

Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa na washirika wake leo wametoa ombi la msaada zaidi wa dola milioni 132.9 ili kuisaidia Niger.

Fedha hizo zitatumika kufadhili mpango wa msaada wa kibinadamu katika nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi ambayo kwa sasa inakabiliwa na baa la njaa.  Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA, Upungufu wa chakula na utapia mlo umewaathiri watu takribani milioni 4.1.

Jumla ya dola milioni 190.7 zinahitajika ,lakini dola milioni 57.8 kati ya hizo zimepatikana na hivyo zinazopungua ni dola milioni 132.9. Pamoja na kipaumbele cha serikali jopo la watoa misaada ya kibinadamu nchini humo wanatoa kipaumbele katika kupatikana chakula na msaada, lishe,msaada wa afya, maji na usafi.

Serilaki ya Niger imesema inakabiliwa na baa la njaa na mwezi uliopia ilitoa ombi la msaada wa kimataifa kuinusuru nchi hioyo na watu wake.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter