Uchaguzi nchini Sudan utafanyika kama ilivyopangwa yasema tume

Uchaguzi nchini Sudan utafanyika kama ilivyopangwa yasema tume

Tume ya uchaguzi nchini Sudan imesema uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi huu nchini humo hautocheleweshwa licha ya chama cha upinzania kususia.

Moja ya masharti yaliyotolewa na chama cha upinzani cha umma ni kuchelewesha uchaguzi kwa takribani wiki nne ili taasisi mpya iundwe kusimamia tume ya uchaguzi. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa uchaguzi kufanyika nchini Sudan tanngu mwaka 1986.

Vyama vingi aidha vimetishia kujiondoka au tayari vimeshajiengua kwenye uchaguzi huo. Kwa mujibu wa msemaji wa tume ya uchaguzi nchini humo Abdallah Ahmed Abdullah uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa kati ya tarehe 11 hadi 13 ya mwezi huu.