Katibu mkuu wa UM ahitimisha ziara Uzubekstan na sasa yuko Tajikistan

Katibu mkuu wa UM ahitimisha ziara Uzubekstan na sasa yuko Tajikistan

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amehitimisha ziara yake nchini Uzubekistan na kuelekea Tajikistan.

Akiwa kwenye kiwanja cha ndege cha Tashkent tayari kwa kuondoka bwana Ban amezungumza na waandishi wa habari na kutoa wito kwa serikali kuimarisha rekodi yake ya haki za binadamu.

Kabla ya hapo alitoa hotuba kwenye chuo kikuu cha kimataifa cha uchumi na diplomasia mjini Tashkent.

Ameisifia nchi ya Uzubekistan kwa hatua iliyopiga kukabiliana na mdororo wa kiuchumi.Hivi sasa bwana Ban ameshaondoka kuelekea Tajikistan na amewasili tayari.