Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwendesha mashitaka wa ICC aeleza mipango ya uchunguzi atakaoufanya Kenya

Mwendesha mashitaka wa ICC aeleza mipango ya uchunguzi atakaoufanya Kenya

Mwendesha mashitaka katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC iliyoko The Hague Uholanzi, Luis Moreno-Ocampo ameainisha jinsi atakavyoendesha uchunguzi wa uhalifu unaodaiwa kufanyika Kenya baada ya utata wa matokeo ya uchaguzi wa Rais mwaka 2007.

Bwana Ocampo amefanya mkutano na waandishi wa habari na amesema kuna orodha ya washukiwa 20. Ameongeza kila mtu mmoja kati ya watatu ana kesi mbili na watazingatia wale waliohusika hasa kwa mujibu wa ushahidi walioupata na watakaoukusanya kwa njia ya haki.

Amesema leongo lao ni kumaliza uchunguzi mwaka huu wa 2010 na kuwasilisha kesi yao mbele ya majaji ambao wataamua endapo watu hao wana hatia ama la. Huu ni mchakato wa kisheria amesema Ocampo.