Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya dharura yameanza Sudan ili kunusuru uchaguzi wa mwezi huu

Mazungumzo ya dharura yameanza Sudan ili kunusuru uchaguzi wa mwezi huu

Mjumbe maalumu wa Marekani nchini Sudan Jenerali Scott Gration ameanza mazungumzo ya dharura ili kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa mjini Khartoum.

Madhumuni ya mazungumzo hayo ni kujaribu kunusuru uchaguzi wa kihistoria unaotarajiwa kufanyika mwezi huu baada ya mgombea rasmi wa chama cha upinzani cha SPLM Yasir Arman kujiondoa kwenye uchaguzi huo.


Kwa mujibu wa bwana Arman hali ya sasa ya usalama katika jimbo la Darfur hairuhusu uchauzi huo kufanyika kwa uhuru na haki. Mpango maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMIS umesem unajitahidi kwa kila njia kuisaidia Sudan kufanya uchaguzi ulio huru na wa haki.