ILO imetoa wito wa kuwepo na mfumo wa haki kwa wafanyakazi wahamiaji

ILO imetoa wito wa kuwepo na mfumo wa haki kwa wafanyakazi wahamiaji

Utafiti uliofanywa na shirika la kazi duniani ILO wakati huu wa mtafaruku wa kiuchimi duniani umeainisha kuwa kuna haja ya kuwa na mtazamo wa haki ili kuwapa usawa wafanyakazi wahamiaji milioni 105 kote duniani.

Utafiti huo mpya waliouita International Labour Migration unaozingatia mtazamo wa haki, umetathmini hali ya mfanyakazi muhamiaji kimataifa, athari zake anakotoka muhamiaji huyo na nchi anayokwenda, na mazingira ya kazi anayokabiliana nayo.

Utafiti huo pia umeangalia ni jinsi gani viwango vinaweza kutumika kuunda na kutekeleza sera za wafanyakazi wahamiaji. Ibrahim Awad wa ILO anafafanua