Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wiki chache zijazo ni muhimu sana katika historia ya Sudan

Wiki chache zijazo ni muhimu sana katika historia ya Sudan

Mwakilishi mpya wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Haile Menkerios amesema wiki chache zijazo ni muhimu sana katika historia ya Sudan tangu nchi hiyo ipate uhuru.

Katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari mjini Khartoum Menkerios amesema kufanyika kwa uchaguzi mkuu uliopangwa mwezi ujao kutakuwa chachu kubwa katika utekelezaji wa mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 2005 na kumaliza vita vya miongo miwili baiana ya Kaskazini na Kusini.

Ameongeza kuwa uchaguzi huo utakaofanyika tarehe 11 hadi 18 Aprili ni lazima uzingatie demokrasia. Mpango wa Umoja wa mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMIS unatoa msaada wa ushauri na kiufundi hususani Sudan kusini katika mipango ya uchaguzi. Umeshatoa mafunzo kwa polisi 24,000, 17, 000 kutoka Kaskazini na 7000 kutoka Kusini.