Skip to main content

Shirikisho la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu kuisaidia Niger

Shirikisho la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu kuisaidia Niger

Shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu IFRC imetoa wito wa msaada wa dola zaidi ya laki tisa ili kusaidia kukabiliana na hali ya upungufu wa chakula iliyotokana na mavuno mabaya mwaka jana nchini Niger.

Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na serikali ya Niger, zaidi ya nusu ya watu wote milioni 15 nchini humo wanakabiliwa na upungufu wa chakula uliosababishwa na mvua za masika kutonyesha ipasavyo.

IFRC inasema idadi ya watoto waliolazwa katika vituo vya lishe kutokana na utapia mlo ni asilimia 60 kwa mezi Januari mwaka huu, ambayo ni kubwa ikilinganishwa na wakati kama huu mwaka jana.

Lengo la IFRC ni kukiwezesha chama cha msalaba mwekundu Niger kusaidia watu laki tatu katika vijiji 120 kwenye mikoa ya Diffa, Zinder na Tahoua.