Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya maji duniani, na maji ni haki ya kila mmoja

Leo ni siku ya maji duniani, na maji ni haki ya kila mmoja

Leo ni siku ya maji duniani na ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNFPA katika kuazimisha siku hii, inasema kuwekeza katika maji safi kutakuwa na manufaa ya kuhakikisha mzunguko wa maisha ulio bora na jamii nzima kwa ujumla.

Ripoti hiyo iloyotolewa mjini Nairobi Kenya pia inasema uwekezaji usio na gharama kubwa wa dola milioni 20 katika teknolojia, kama vile ya mipira ya umwagiliaji na pampu, kutazitoa familia milioni 100 za wakulima kutoka kwenye umesikini uliokithiri.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa la msingi ni kusafisha maji, na juhudi ni kupata suluhisho la maji safi na salama, pia kukarabati mabomba yaliyopasuka ambayo yanavujisha maji na mitambo ya maji taka, kutasaidia sio tuu kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana bali kutapunguza uharibifu wa mazingira na kutatoa ajira.