Skip to main content

Ban Ki-moon ataka Israel kuondoa vikwazo dhidi ya ukanda wa Gaza

Ban Ki-moon ataka Israel kuondoa vikwazo dhidi ya ukanda wa Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekosoa vikwazo vya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza alipokuwa ziarani jana kwenye ukanda huo uliosambaratishwa na vita.

Bwana Ban amesema vikwazo hivyo vinawafanya raia wa Gaza kupata mateso yasiyostahili. Ziara ya Ban imekuwa na lengo la kuchagiza kufufuliwa kwa mazungumzo ya amani baiana Israel na Palestina yaliyovunjika mwezi Desemba na Januari mwaka huu.

Ban amesema vikwazo vya Israel dhidi ya Gaza pia vinazuia biashara halali na kuchangia biashara haramu, vinawanyiama haki raia wanaostahili na kuwapa uwezo wenye itikadi kali kutekeleza matakwa yao.