Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon amekutana na viongozi wa Urusi

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon amekutana na viongozi wa Urusi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mikutano na Rais wa Urus Demitry Medvedev na waziri wa mambo ya nje Sergei Lavrov mjini Moscow.

Akiwa nchini humo pia bwana Ban ametia saini azimio la ushirikiano na shirika la mkataba wa pamoja wa masuala ya usalama CSTO. Katibu mkuu wa CSTO Nikolai Bordyuzha amesema shirika lake kwa ombi la Umoja wa Mataifa linaweza kutuma vikosi vya kulinda amani hata nje ya maeneo yake.

Amesema wanaweza kupeleka vikosi vyao hata Afrika kwa mfano. Ban pia atahudhuria mkutano wa masuala ya mashariki ya kati utakaofanyika mjini Moscow.