Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu milioni 200 wamekwepa kuishi katika mitaa ya mabanda

Zaidi ya watu milioni 200 wamekwepa kuishi katika mitaa ya mabanda

Ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT inayoelezea hali ya miji duniani kwa mwaka 2010/2011 inasema, watu milioni 227 wameepuka maisha ya mitaa ya mabanda katika muongo mmoja uliopita.

Ripoti inasema maendeleo hayo ni kutokana na juhudi kubwa za ujenzi wa nyumba zilizofanywa na Uchina na India. Hata hivyo ujenzi huo wa nyumba haukuzingatia ongezeko la watu na pia idadi ya watu wanaokimbia vijijini kwenda mijini.

Pamoja na kwamba hatua imepigwa lakini kwa ujumla idadi ya watu wanaoishi katika mitaa ya mabanda inaonekana kuongezeka kutoka milioni 776.7 hadi milioni 827.6 kuanzia mwaka 2000 hadi 2010.