Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yashikamana kupigania haki za wasichana

Mashirika ya UM yashikamana kupigania haki za wasichana

Wajumbe wa Umoja wa mataifa wa kundi linalopigania haki za wasichana Adolescent Girls Task Force, leo kwa pamoja wametoa ombi la kuongeza juhudi la kupigania haki za binadamu kwa waasichana.

Katika miaka mitano ijayo kundi hilo linalojumuisha ILO, UNESCO, UNFPA, UNICEF, UNIFEM na WHO wataongeza msaada wao kwa nchi zinazoendelea ili kuimarisha sera zao na miradi mbalimbali ambayo itasaidia kufikia malengo ya ukombozi wa wasichana hasa wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 14.

Wanasema wasichana wengi kati ya milioni 600 wanaishi katika nchi zinazoendelea na hawajumuishwi katika mipango na sera za taifa, japo katika masuala kama elimu hatua imepigwa. Elizabeth Gibbons ni naibu mkurugenzi wa sera na mipango wa UNICEF