Mshauri wa UM wa kuzuia mauaji ya kimbari amekwenda Afrika magharibi

Mshauri wa UM wa kuzuia mauaji ya kimbari amekwenda Afrika magharibi

Mshauri maalumu wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya Kimbari amekwenda Afrika ya magharibi leo.

Mwakilishi huyo atazuru Guinea, Nigeria na Ghana. Katika ziara yake atakutana na viongozi wa nchi hizo ili kujadili masuala mbalimbali ikiwemo jinsi vyombo na taasisi za kikanda zinavyoweza kuzua mauaji ya kimbari.

Afrika ya Magharibi imekuwa ikikumbwa na migogoro ikiwemo ya kisiasa, kijamii na hata kidini ambayo inakatili maisha ya watu wengi, kuwaacha maelfu wakiishi kwa woga na wengine kuyakimbia makazi yao.