Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la ubakaji DRC linaathiri wanawake na jamii kwa ujumla

Tatizo la ubakaji DRC linaathiri wanawake na jamii kwa ujumla

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu UNFPA linasema matatizo ya ukatili wa kimapenzi dhidi ya wanawake nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni makubwa na athari zake sio kwa wanawake tuu bali hata kwa jamii nzima.

Kwa mujibu wa afisa wa UNFPA Maha Mouna tatizo hilo ni kubwa zaidi katika mikoa ya Kivu ya Kaskazini na Kusini mashariki mwa nchi hiyo, ambako bado vita baina ya majeshi ya serikali na makundi ya wanamgambo wa Kihutu vinaendelea.

Ameongeza kuwa ukatili huo licha ya kumuathiri mwanamke aliyebakwa kisaikolojia na kumuharibia maisha , pia unaathiri watoto wa wanawake hao na jamii nzima kwa ujumla.